WATUHUMIWA 41 MBALONI KWA KOSA LA KUIBA NYETI

WATUHUMIWA 41 MBALONI KWA KOSA LA KUIBA NYETI

Taarifa ya leo Mei 07, 2026 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi, Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Kaster Ngonyani imeeleza kuwa watuhumiwa 14 wamekamatwa kwa makosa tofauti ya mauaji huku wengine 7 wakikamatwa wakiwa na silaha haramu 4 aina ya gobore, pamoja nyama kiasi cha kilo 11 ya mnyama pori Nyati na kilo 40 ya Twiga.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa watuhumiwa 3 walikamatwa wakiwa na kilo 4 na kete 101 za dawa za kulevya aina ya bangi pamoja na huku watuhumiwa 07 wakitiwa mbaroni wakiwa na jumla ya lita 102 za pombe ya moshi (gongo) wakati wengine 10 wakikamatwa wakiwa na vitu mbalimbali vya wizi.

Vitu hivyo vya wizi ni pamoja na pikipiki moja aina ya SANLG yenye namba ya usajili MC 578 EWY, televisheni 01, aina ya Sundar, Solar panel 01 aina ya Sundar, redio 01 aina ya Aboder, speaker 04 za redio, magodoro 02 yenye ukubwa tofauti, computer aina ya DELL na HP, ndoo 04 za plastiki, jaba 06, cherehani 01 aina ya Butterfly, nondo rola 07 na vipande 35, mitungi ya gesi, jiko 01 la gesi na jora mbili za vitambaa.