WATAZAME TEMBO WAKUBWA WA HIFADHI YA TAIFA KATAVI

WATAZAME TEMBO WAKUBWA WA HIFADHI YA TAIFA KATAVI

WATAZAME TEMBO WAKUBWA WA HIFADHI YA KATAVI: Hifadhi ya Taifa ya Katavi inajivunia utajiri mkubwa wa tembo wa Afrika, wanaopatikana kwa makundi makubwa katika maeneo ya mito na tambarare za Katuma.

Utajiri wake wa kipekee unatokana na Idadi kubwa na makundi makubwa yanayoonekana hasa wakati wa kiangazi wanapokusanyika karibu na vyanzo vya maji.

Mazingira asilia na tulivu, yasiyo na msongamano wa watalii, yanayowezesha tembo kuishi kwa uhuru mkubwa.

Ukubwa wa eneo la hifadhi (km² 4,471) unaotoa nafasi ya kutosha kwa tembo kuhama na kutafuta chakula kulingana na misimu.

Kwa sababu hiyo, Katavi ni moja ya maeneo bora nchini Tanzania kwa kushuhudia tembo katika mazingira yao halisi ya porini, jambo linaloipa hifadhi hii hadhi ya kipekee katika utalii wa wanyamapori.