DKT.MWIGULU: MAARIFA YA NANENANE YATUMIKE KUONGEZA TIJA

DKT.MWIGULU: MAARIFA YA NANENANE YATUMIKE KUONGEZA TIJA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka Wananchi kutumia maarifa wanayoyapata katika Maonesho ya Kilimo Nanenane na kuyafanyia kazi ili kuongeza tija katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.

Dkt. Mwigulu amesema hayo leo Agosti 1, 2026 wakati akifungua rasmi Maonesho ya Kilimo Nanenane katika Viwanja vya Dkt. John Malecela Jijini Dodoma ambapo ameeleza kuwa maonesho hayo yanatoa fursa kwa Wananchi kujifunza teknolojia na mbinu bora za uzalishaji zitakazosaidia kuinua uchumi na kuongeza uzalishaji.

Aidha, amewataka Watumishi wa umma pamoja na Wataalamu wa Serikali kuongeza uwajibikaji katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi ili Wananchi wanufaike zaidi na uwekezaji unaofanywa na Serikali kupitia ongezeko la bajeti katika sekta hizo.